Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 42:1 - Swahili Revised Union Version

1 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kama ayala anavyoonea shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku, Ee Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu.

Tazama sura Nakili




Zaburi 42:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;


Nafunua kinywa changu nikihema, Maana nazitamani amri zako.


Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.


Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.


Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.


Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.


Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.


Sikieni haya, enyi mataifa yote; Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani.


BWANA, umeiridhia nchi yako, Umewarejesha mateka wa Yakobo.


Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu.


Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako.


Na wana wa Kora; ni Asiri, na Elkana, na Abiasafu; hizo ni jamaa za hao Wakora.


Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;


nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.


Hata hivyo, hao wana wa Kora hawakufa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo