Abrahamu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo dume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Abrahamu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
Hesabu 23:3 - Swahili Revised Union Version Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lolote atakalonionesha nitakuambia. Akaenda hadi mahali peupe juu ya kilima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima. Biblia Habari Njema - BHND Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Halafu Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende. Labda Mwenyezi-Mungu atakutana nami. Chochote atakachonionesha nitakuja kukuambia.” Basi, Balaamu akaenda peke yake juu ya kilele cha mlima. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninaenda kando. Huenda Mwenyezi Mungu atakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda kando. Huenda bwana atakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka. BIBLIA KISWAHILI Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lolote atakalonionesha nitakuambia. Akaenda hadi mahali peupe juu ya kilima. |
Abrahamu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo dume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Abrahamu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu.
Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile BWANA atialo kinywani mwangu?
Akamwambia Balaki, Simama hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami nitaonana na BWANA kule.
Balaki akafanya kama Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng'ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
Lakini Balaamu akajibu akamwambia Balaki, Je! Sikukuambia ya kwamba, Kila neno BWANA atakalolisema sina budi kulitenda?
Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng'ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza BWANA kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, ili kupiga bao, bali alielekeza uso wake jangwani.
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
lakini sikukubali kumsikiliza Balaamu; kwa hiyo akafululiza kuwabariki; basi nikawatoa katika mkono wake.