Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 24:1 - Swahili Revised Union Version

1 Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza BWANA kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, ili kupiga bao, bali alielekeza uso wake jangwani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena, akawa anaangalia jangwani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena, akawa anaangalia jangwani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena, akawa anaangalia jangwani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi Balaamu alipoona imempendeza Mwenyezi Mungu kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi Balaamu alipoona imempendeza bwana kubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza BWANA kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, ili kupiga bao, bali alielekeza uso wake jangwani.

Tazama sura Nakili




Hesabu 24:1
13 Marejeleo ya Msalaba  

Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Nendeni zenu hadi nchi yenu; kwa maana BWANA amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi.


Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.


Akamwambia Balaki, Simama hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami nitaonana na BWANA kule.


Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.


Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!


Basi Balaki akamchukua Balaamu akaenda naye mpaka kilele cha mlima Peori, mahali paelekeapo upande wa nyika iliyo chini yake.


Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lolote atakalonionesha nitakuambia. Akaenda hadi mahali peupe juu ya kilima.


Basi Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, akasongeza sadaka ng'ombe dume na kondoo dume juu ya kila madhabahu.


Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie BWANA dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hiyo pigo lilikuwa katika mkutano wa BWANA.


Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie kikwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.


Na sasa, angalia, ninajua ya kuwa hakika utakuwa mfalme, na ufalme wa Israeli utafanyika imara mkononi mwako.


Basi Sauli akaondoka, akashuka nyikani kwa Zifu, naye alikuwa na watu elfu tatu, wateule wa Israeli, pamoja naye, ili kumtafuta Daudi katika nyika ya Zifu.


Ndipo Sauli akamwambia Daudi, Ubarikiwe, Daudi, mwanangu; utatenda mambo makuu, tena hakika yako utashinda. Basi, Daudi akaenda zake; Sauli naye akarudi kwao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo