Hesabu 20:3 - Swahili Revised Union Version Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingekuwa heri kama tungekufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za BWANA! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waliwalalamikia wote wakisema, “Afadhali tungekufa pamoja na ndugu zetu mbele ya hema la Mwenyezi-Mungu! Biblia Habari Njema - BHND Waliwalalamikia wote wakisema, “Afadhali tungekufa pamoja na ndugu zetu mbele ya hema la Mwenyezi-Mungu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waliwalalamikia wote wakisema, “Afadhali tungekufa pamoja na ndugu zetu mbele ya hema la Mwenyezi-Mungu! Neno: Bibilia Takatifu Watu wakagombana na Musa, na kusema, “Laiti tungekufa ndugu zetu walipokufa mbele za Mwenyezi Mungu! Neno: Maandiko Matakatifu Watu wakagombana na Musa, na kusema, “Laiti tungelikufa wakati ndugu zetu walipoanguka na kufa mbele za bwana! BIBLIA KISWAHILI Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingekuwa heri kama tungekufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za BWANA! |
Kwa hiyo hao watu wakamgombeza Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwa nini mnanigombeza? Mbona mnamjaribu BWANA?
Heri wale waliouawa kwa upanga Kuliko wao waliouawa kwa njaa; Maana hao husinyaa, wakichomwa Kwa kukosa matunda ya mashamba.
Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza hadi viunga vya kambi.
Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?
Basi waliokufa kwa tauni walikuwa elfu kumi na nne na mia saba, zaidi ya hao waliokufa katika jambo la Kora.