Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 20:4 - Swahili Revised Union Version

4 Mbona mmewaleta kusanyiko la BWANA hadi jangwani hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kwa nini mlituleta sisi jumuiya ya Mwenyezi-Mungu huku jangwani? Je, mlituleta ili tufe pamoja na mifugo yetu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kwa nini mlituleta sisi jumuiya ya Mwenyezi-Mungu huku jangwani? Je, mlituleta ili tufe pamoja na mifugo yetu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kwa nini mlituleta sisi jumuiya ya Mwenyezi-Mungu huku jangwani? Je, mlituleta ili tufe pamoja na mifugo yetu?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa nini mmewaleta jumuiya ya Mwenyezi Mungu kwenye jangwa hili, ili tufe humu, sisi na mifugo yetu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa nini mmeileta jumuiya ya bwana kwenye jangwa hili, ili tufe humu, sisi na mifugo yetu?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Mbona mmewaleta kusanyiko la BWANA hadi jangwa hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu?

Tazama sura Nakili




Hesabu 20:4
13 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri.


wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.


Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?


wakawaambia, BWANA awaangalie na kuamua; kwa kuwa mmefanya harufu yetu kuwa chukizo mbele ya Farao, na mbele ya watumishi wake, mkatia upanga mikononi mwao, watuue.


lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hadi hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa BWANA aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?


Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;


Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.


Lakini siku ya pili yake mkutano wote wa wana wa Israeli wakamnung'unikia Musa, na Haruni, wakasema, Ninyi mmewaua watu wa BWANA.


Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka.


lakini hapo walipokwea kutoka Misri, na Israeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu, na Kadeshi;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo