Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.
Hesabu 2:3 - Swahili Revised Union Version Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa bendera ya kambi ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua watakuwa kikundi cha watu walio chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu, Biblia Habari Njema - BHND “Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua watakuwa kikundi cha watu walio chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Wale watakaopiga kambi upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua watakuwa kikundi cha watu walio chini ya bendera ya Yuda na kiongozi wao atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu, Neno: Bibilia Takatifu Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya beramu yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua: kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu. BIBLIA KISWAHILI Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea mawio ya jua, ndio wale wa bendera ya kambi ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu. |
Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.
Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Ingawa Yuda ndiye aliyekuzwa zaidi miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; haki ile ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu);
Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.
Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha sana, makambi yaliyoko upande wa mashariki yatasafiri. Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha ya pili, makambi yaliyoko upande wa kusini yatasafiri;
Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea maawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa.
Basi aliyetoa matoleo yake siku ya kwanza ni Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda;
na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu.