Hesabu 12:9 - Swahili Revised Union Version Hasira za BWANA zikawaka juu yao; kisha akaenda zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo Mwenyezi-Mungu akawaka hasira dhidi yao, akaondoka, akaenda zake. Biblia Habari Njema - BHND Hapo Mwenyezi-Mungu akawaka hasira dhidi yao, akaondoka, akaenda zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo Mwenyezi-Mungu akawaka hasira dhidi yao, akaondoka, akaenda zake. Neno: Bibilia Takatifu Hasira ya Mwenyezi Mungu ikawaka dhidi yao, akawaacha. Neno: Maandiko Matakatifu Hasira ya bwana ikawaka dhidi yao, akawaacha. BIBLIA KISWAHILI Hasira za BWANA zikawaka juu yao; kisha akaenda zake. |
Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.
Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza hadi viunga vya kambi.
Basi Musa akawasikia watu wakilia katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema yake; na hasira za BWANA zikawaka sana; Musa naye akakasirika.