Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa mataifa mengi
Hesabu 1:33 - Swahili Revised Union Version wale waliohesabiwa katika kabila la Efraimu, walikuwa watu elfu arubaini na mia tano (40,500). Matoleo zaidiBiblia Habari Njema walikuwa watu 40,500. Biblia Habari Njema - BHND walikuwa watu 40,500. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza walikuwa watu 40,500. Neno: Bibilia Takatifu Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu elfu arobaini na mia tano. Neno: Maandiko Matakatifu Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu 40,500. BIBLIA KISWAHILI wale waliohesabiwa katika kabila la Efraimu, walikuwa watu elfu arobaini na mia tano (40,500). |
Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa mataifa mengi
Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.
Katika wana wa Yusufu, maana katika wana wa Efraimu, vizazi vyao kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani,
Katika wana wa Manase, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;
Hawa ndio jamaa wa wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, elfu thelathini na mbili na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao.
Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.