Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
Hesabu 1:22 - Swahili Revised Union Version Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanaume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kutoka kabila la Simeoni kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, Biblia Habari Njema - BHND Kutoka kabila la Simeoni kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kutoka kabila la Simeoni kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini, Neno: Bibilia Takatifu Kutoka wazao wa Simeoni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. Neno: Maandiko Matakatifu Kutoka wazao wa Simeoni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao. BIBLIA KISWAHILI Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanaume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; |
Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
Akaenda kando, akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao.
Na wana wa Simeoni; Yemueli na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli, mwana wa mwanamke Mkanaani.
Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana.
wale waliohesabiwa katika kabila la Reubeni, walikuwa watu elfu arubaini na sita na mia tano (46,500) mmoja mmoja.
wale waliohesabiwa katika kabila la Simeoni, walikuwa watu elfu hamsini na tisa na mia tatu (59,300).
Wa kabila la Simeoni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Lawi elfu kumi na mbili. Wa kabila la Isakari elfu kumi na mbili.