Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.
Hagai 1:7 - Swahili Revised Union Version BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Fikirini kama mnafanya sawa! Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Fikirini kama mnafanya sawa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Fikirini kama mnafanya sawa! Neno: Bibilia Takatifu Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Zitafakarini vyema njia zenu. Neno: Maandiko Matakatifu Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu. BIBLIA KISWAHILI BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. |
Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.
Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.
Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema BWANA.
Na sasa nawaomba, tafakarini; tangu siku hii na siku zilizopita; kabla jiwe halijatiwa juu ya jiwe katika nyumba ya BWANA;
Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.