Ndipo mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani, na makuhani wengine, akawauliza, Mbona hamtengenezi mabomoko ya nyumba? Basi sasa msipokee tena fedha kwa hao mwajuao, lakini itoeni kwa ajili ya mabomoko ya nyumba.
Hagai 1:2 - Swahili Revised Union Version BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Wakati wa kuijenga upya nyumba ya BWANA haujafika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.” Biblia Habari Njema - BHND Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.” Neno: Bibilia Takatifu Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya Mwenyezi Mungu.’ ” Neno: Maandiko Matakatifu Hivi ndivyo asemavyo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya bwana.’ ” BIBLIA KISWAHILI BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Wakati wa kuijenga upya nyumba ya BWANA haujafika. |
Ndipo mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani, na makuhani wengine, akawauliza, Mbona hamtengenezi mabomoko ya nyumba? Basi sasa msipokee tena fedha kwa hao mwajuao, lakini itoeni kwa ajili ya mabomoko ya nyumba.
Kisha nakala ya barua hiyo ya mfalme Artashasta iliposomwa mbele ya Rehumu, mtawala na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.
Lakini Yuda wakasema, Nguvu zao wapagazi zimedhoofika, bado kuna vifusi tele; hatuwezi kuujenga ukuta.
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Katika mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake nabii Hagai, kusema,
Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.