Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hagai 1:2 - Swahili Revised Union Version

2 BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Wakati wa kuijenga upya nyumba ya BWANA haujafika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya Mwenyezi Mungu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Hivi ndivyo asemavyo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba ya bwana.’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Wakati wa kuijenga upya nyumba ya BWANA haujafika.

Tazama sura Nakili




Hagai 1:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani, na makuhani wengine, akawauliza, Mbona hamtengenezi mabomoko ya nyumba? Basi sasa msipokee tena fedha kwa hao mwajuao, lakini itoeni kwa ajili ya mabomoko ya nyumba.


Kisha nakala ya barua hiyo ya mfalme Artashasta iliposomwa mbele ya Rehumu, mtawala na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha.


Lakini Yuda wakasema, Nguvu zao wapagazi zimedhoofika, bado kuna vifusi tele; hatuwezi kuujenga ukuta.


Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu.


Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.


Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.


Wakati wa kuua, na wakati wa kuponya; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;


Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.


Katika mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake nabii Hagai, kusema,


Ndipo neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,


Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo