Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.
Danieli 6:25 - Swahili Revised Union Version Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi. Biblia Habari Njema - BHND Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha duniani kote: “Mafanikio yawe kwenu sana! Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa, na watu wa kila lugha katika nchi yote: “Ninyi na mstawi sana! Swahili Roehl Bible 1937 Kisha mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote na wa koo zote, wao wote wenye ndimi za watu waliokaa katika nchi yote nzima, kwamba: Utengemano wenu na uwe mwingi! |
Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza, kwa wakuu wa mfalme, na wakuu wa mikoa, na wakuu wa kila taifa; kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutiwa mhuri kwa pete yake.
Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na wakuu wa tarafa na wakuu wa mikoa kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi, mikoa mia moja na ishirini na saba, kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.
Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,
Mfalme Nebukadneza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.
ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.