Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 6:25 - Swahili Revised Union Version

25 Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani: “Nawatakieni amani kwa wingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Kisha Mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, na mataifa, na wa kila lugha duniani kote: “Mafanikio yawe kwenu sana!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Kisha Mfalme Dario akawaandikia kabila zote za watu, mataifa, na watu wa kila lugha katika nchi yote: “Ninyi na mstawi sana!

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

25 Kisha mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote na wa koo zote, wao wote wenye ndimi za watu waliokaa katika nchi yote nzima, kwamba: Utengemano wenu na uwe mwingi!

Tazama sura Nakili




Danieli 6:25
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.


Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza, kwa wakuu wa mfalme, na wakuu wa mikoa, na wakuu wa kila taifa; kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutiwa mhuri kwa pete yake.


Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.


Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na wakuu wa tarafa na wakuu wa mikoa kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi, mikoa mia moja na ishirini na saba, kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.


Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoichimba!


BWANA amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.


Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake.


Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,


Mfalme Nebukadneza, kwa watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wanaokaa katika dunia yote; Amani iongezeke kwenu.


ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.


kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.


Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.


Mwongezewe rehema na amani na upendano.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo