Barua kutoka nabii Eliya ilimjia, ikisema, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Kwa kuwa hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda;
Danieli 5:25 - Swahili Revised Union Version Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Maandishi yenyewe ni: ‘MENE, MENE, TEKELI, PARSINI.’ Biblia Habari Njema - BHND “Maandishi yenyewe ni: ‘MENE, MENE, TEKELI, PARSINI.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Maandishi yenyewe ni: ‘MENE, MENE, TEKELI, PARSINI.’ Neno: Bibilia Takatifu “Haya ndio maneno yaliyoandikwa: mene, mene, tekeli, na peresi Neno: Maandiko Matakatifu “Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa: mene, mene, tekeli na peresi Swahili Roehl Bible 1937 Nayo haya maandiko yaliyoandikwa hapa ni kwamba: Mene, Mene, Tekel, U-parsin |
Barua kutoka nabii Eliya ilimjia, ikisema, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, Kwa kuwa hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda;
Fahari yako imeshushwa hadi kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.
Kwa sababu hiyo uovu utakupata; wala hutaweza kuuagua; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa usioujua utakupata kwa ghafla.
Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye.
Ndipo kile kiganja cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.
Je! Hawatainuka ghafla wao watakaokuuma, hawataamka wao watakaokusumbua, nawe utakuwa mateka kwao?
Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Tena pamoja na wewe BWANA atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena BWANA atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.