Amosi 9:5 - Swahili Revised Union Version Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Nili, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, anaigusa ardhi nayo inatetemeka na wakazi wake wanaomboleza; dunia nzima inapanda na kushuka kama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri. Biblia Habari Njema - BHND Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, anaigusa ardhi nayo inatetemeka na wakazi wake wanaomboleza; dunia nzima inapanda na kushuka kama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, anaigusa ardhi nayo inatetemeka na wakazi wake wanaomboleza; dunia nzima inapanda na kushuka kama kujaa na kupwa kwa mto Nili wa Misri. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, na wote wanaoishi ndani yake wakaomboleza: nayo nchi yote huinuka kama Mto Naili, kisha hushuka kama mto wa Misri; Neno: Maandiko Matakatifu Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza: nayo nchi yote huinuka kama Naili, kisha hushuka kama mto wa Misri; BIBLIA KISWAHILI Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Nili, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri. |
Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye Akuombe awapo katika dhiki. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye.
Hata lini itaomboleza nchi, na kukauka majani ya nchi yote? Kwa ajili ya mabaya yao wakaao ndani yake, wanyama wameangamia na ndege pia; kwa sababu walisema, Yu kipofu katika njia zetu.
Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa.
Kwa ajili ya hayo, je! Haitatetemeka nchi, na kuomboleza kila mtu akaaye ndani yake? Naam, itainuka yote pia kama huo Mto; nayo itataabika na kupwa tena kama Mto wa Misri.
Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.
Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.
Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.
mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.