Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Amosi 2:4 - Swahili Revised Union Version

Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamepuuza sheria zangu, wala hawakufuata amri zangu. Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamepuuza sheria zangu, wala hawakufuata amri zangu. Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamepuuza sheria zangu, wala hawakufuata amri zangu. Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Yuda, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu wameikataa Torati ya Mwenyezi Mungu na hawakuzishika amri zake, kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, miungu ambayo babu zao waliifuata.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hili ndilo asemalo bwana: “Kwa dhambi tatu za Yuda, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu wameikataa Torati ya bwana na hawakuzishika amri zake, kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, miungu ambayo babu zao waliifuata.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Amosi 2:4
53 Marejeleo ya Msalaba  

Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya BWANA, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe.


Basi ikawa, Amazia alipokwisha rudi kutoka kuwaua Waedomi, alileta miungu ya wana wa Seiri, akaisimamisha kuwa miungu yake, akaisujudia, akaifukizia uvumba.


Wala msiwe kama baba zenu, na kama ndugu zenu, waliomwasi BWANA, Mungu wa baba zao, hata akawatoa kuwa ukiwa, kama mwonavyo.


Tumetenda maovu mengi juu yako, wala hatukuzishika amri, wala sheria, wala hukumu, ulizomwamuru Musa, mtumishi wako.


Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.


Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;


Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?


Ndipo utakapowaambia, Ni kwa sababu baba zenu wameniacha mimi, asema BWANA, na kuwafuata miungu mingine, na kuwatumikia, na kuwaabudu, wakaniacha mimi, wasiishike torati yangu;


na ninyi mmetenda mabaya kupita baba zenu; maana angalieni, mnaenda kila mmoja wenu kwa ushupavu wa moyo wake mbaya, msinisikilize mimi;


Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo katika malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika.


Sikia, Ee nchi; tazama, nitaleta mabaya juu ya watu hawa, naam, matunda ya mawazo yao, kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa.


nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi.


Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la BWANA, wana akili gani ndani yao?


bali wameenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe, na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao.


Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia yake mbaya, na kuhifadhika;


Lakini nyumba ya Israeli waliniasi jangwani; hawakuenda katika amri zangu, wakazikataa hukumu zangu, ambazo mwanadamu ataishi kwazo, kama akizitenda; na sabato zangu walizitia unajisi sana; ndipo nikasema, Nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani, ili niwaangamize.


kwa sababu walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika amri zangu, wakazitia unajisi sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao.


Kisha nikawaambia watoto wao jangwani, Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao.


kwa sababu hawakuzitekeleza hukumu zangu, bali walizikataa amri zangu, nao walizitia unajisi sabato zangu, na macho yao yaliandama vinyago vya baba zao.


Basi, uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Je! Mnajitia unajisi kwa kuzifuata njia za baba zenu? Mnakwenda kufanya uasherati kwa kuyafuata machukizo yao?


Na manabii wake wamewapakia chokaa isiyokorogwa vema, wakiwa na maono ya udanganyifu, na kuwatabiria maneno ya uongo, wakisema, Bwana MUNGU asema hivi; iwapo BWANA hakusema neno.


Umevidharau vitu vyangu vitakatifu, umezitia unajisi sabato zangu.


BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.


Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu;


Tena, Ee Yuda, wewe umeandikiwa mavuno, hapo nitakapowarudisha wafungwa wa watu wangu.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma;


Ni ninyi tu niliowajua katika jamaa zote zilizo duniani; kwa sababu hiyo nitawapatiliza ninyi maovu yenu yote.


Kwa maana matajiri wake wamejaa jeuri, na wenyeji wake wamesema uongo, na ulimi wao una udanganyifu kichwani mwao.


Sanamu ya kuchonga yafaa nini, baada ya aliyeifanya ameichonga? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini, hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanya sanamu zisizoweza kusema?


Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.


Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.


Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;


Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamuacha BWANA, wala hawakumtumikia yeye.