2 Timotheo 4:4 - Swahili Revised Union Version nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo. Biblia Habari Njema - BHND Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo. Neno: Bibilia Takatifu Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo. Neno: Maandiko Matakatifu Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo. BIBLIA KISWAHILI nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. |
wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Lakini hao walikataa kusikiliza, wakageuza bega lao, wakaziba masikio yao ili wasisikie.
Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na kikomo, zinazozua maswali wala si mpango wa Mungu ulio katika imani; basi uwaambie hivyo.
Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na mazungumzo yasiyo ya kimungu, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo;
Waijua habari hii, ya kuwa wote walio wa Asia waliniepuka, ambao miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene.
Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.