2 Samueli 22:5 - Swahili Revised Union Version Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira, mafuriko ya maangamizi yalinivamia; Biblia Habari Njema - BHND “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira, mafuriko ya maangamizi yalinivamia; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira, mafuriko ya maangamizi yalinivamia; Neno: Bibilia Takatifu Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. Neno: Maandiko Matakatifu “Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. BIBLIA KISWAHILI Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. |
Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.
Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, basi jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.