2 Samueli 22:40 - Swahili Revised Union Version Maana umenijaza nguvu ya kupigana vita; Ukawafanya adui zangu wafifie chini yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita; uliwaporomosha adui chini yangu. Biblia Habari Njema - BHND Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita; uliwaporomosha adui chini yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita; uliwaporomosha adui chini yangu. Neno: Bibilia Takatifu Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. Neno: Maandiko Matakatifu Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. BIBLIA KISWAHILI Maana umenijaza nguvu ya kupigana vita; Ukawafanya adui zangu wafifie chini yangu. |
Mwamba wangu na ngome yangu, Nguzo yangu na mwokozi wangu Ngao yangu ninayemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu.
Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakuimarisha ijapokuwa hukunijua;
Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha katika nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Ndipo wakaenda Keila, Daudi na watu wake, wakapigana na hao Wafilisti, wakateka nyara ng'ombe zao, na kuwaua uuaji mkuu. Hivyo Daudi akawaokoa watu wa Keila.