2 Samueli 22:23 - Swahili Revised Union Version Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu; Na kuhusu amri zake, sikuziacha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimeshika maagizo yake yote, sikuacha kufuata masharti yake. Biblia Habari Njema - BHND Nimeshika maagizo yake yote, sikuacha kufuata masharti yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimeshika maagizo yake yote, sikuacha kufuata masharti yake. Neno: Bibilia Takatifu Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. Neno: Maandiko Matakatifu Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. BIBLIA KISWAHILI Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu; Na kuhusu amri zake, sikuziacha. |
Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiishi katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama.
moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kulia wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli.
Na itakuwa, kwa sababu mnazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;
Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo.