2 Samueli 22:14 - Swahili Revised Union Version BWANA alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye Juu akaitoa sauti yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni, Mungu Mkuu akatoa sauti yake. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni, Mungu Mkuu akatoa sauti yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni, Mungu Mkuu akatoa sauti yake. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. Neno: Maandiko Matakatifu bwana alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. BIBLIA KISWAHILI BWANA alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye Juu akaitoa sauti yake. |
nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.
Naye BWANA atawasikizisha watu sauti yake ya utukufu, naye atawaonesha jinsi mkono wake ushukavyo, na ghadhabu ya hasira yake, na mwako wa moto uangamizao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya barafu.
Na sauti ya mabawa ya makerubi ikasikiwa, hata katika ua wa nje, kama sauti ya Mungu Mwenyezi, asemapo.
Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.
Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.
Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; lakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.