Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 2:10 - Swahili Revised Union Version

10 Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande; atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni. Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote; atampa nguvu mfalme wake ataukuza uwezo wa mteule wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande; atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni. Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote; atampa nguvu mfalme wake ataukuza uwezo wa mteule wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande; atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni. Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote; atampa nguvu mfalme wake ataukuza uwezo wa mteule wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 wale wampingao Mwenyezi Mungu wataharibiwa kabisa. Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; Mwenyezi Mungu ataihukumu miisho ya dunia. “Atampa nguvu mfalme wake, na kuitukuza pembe ya mpakwa mafuta wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 wale wampingao bwana wataharibiwa kabisa. Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; bwana ataihukumu miisho ya dunia. “Atampa nguvu mfalme wake, na kuitukuza pembe ya mpakwa mafuta wake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 2:10
50 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye Juu akaitoa sauti yake.


Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakiimarisha milele.


Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, BWANA wa majeshi asema hivi, Nilikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;


Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?


Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu.


Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.


Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,


Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.


Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.


Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake; Atamjibu toka mbingu zake takatifu, Kwa matendo makuu ya wokovu Ya mkono wake wa kulia.


Hawa wanataja magari na hawa farasi, Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.


Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.


BWANA ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.


Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.


Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe, Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.


Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.


Nitaweka mkono wake juu ya bahari, Na mkono wake wa kulia juu ya mito.


Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.


Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.


BWANA, mkono wako wa kulia umepata fahari ya uwezo, BWANA, mkono wako wa kulia wawasetaseta adui.


Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.


Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.


Naye atajiliwa na BWANA wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.


Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu.


Mmoja ataniambia, Kwa BWANA, peke yake, iko haki na nguvu; naam, watu watamwendea yeye, na wote waliomkasirikia watatahayarika.


Siku ile nitawachipushia nyumba ya Israeli pembe, nami nitakujalia kufumbua kinywa kati yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Kisha Mfalme atawaambia wale walioko katika mkono wake wa kulia, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;


Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.


Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.


Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa muwachinje mbele yangu.


habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee malipo ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, yawe ni mema au mabaya.


Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arubaini.


Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, BWANA ameweka mfalme juu yenu.


Je! Leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba atume ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu mlioufanya machoni pa BWANA, ni mwingi sana, kwa kujitakia mfalme.


Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akatuma ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia.


Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi wake, nilitwaa ng'ombe wa nani? Au nilitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi.


Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.


BWANA akamwambia Samweli, utamlilia Sauli hadi lini, kwa kuwa mimi nimemkataa asiwatawale Waisraeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakutuma kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.


Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; lakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo