2 Petro 3:5 - Swahili Revised Union Version Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na dunia zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji; Biblia Habari Njema - BHND Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na dunia zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu hao, kwa makusudi, husahau kwamba zamani Mungu alinena, nazo mbingu na dunia zikaumbwa. Dunia iliumbwa kutoka katika maji na kwa maji; Neno: Bibilia Takatifu Lakini wao kwa makusudi hupuuza ukweli huu, kwamba kwa neno la Mungu mbingu zilikuwa tangu zamani, nayo dunia ilifanyizwa kutoka ndani ya maji na kwa maji. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wao kwa makusudi hupuuza ukweli huu, ya kwamba kwa neno la Mwenyezi Mungu mbingu zilikuwepo tangu zamani, nayo dunia ilifanyizwa kutoka ndani ya maji na kwa maji. BIBLIA KISWAHILI Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; |
Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.