nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani.
1 Samueli 5:10 - Swahili Revised Union Version Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu mpaka Ekroni. Ikawa, sanduku la Mungu lilipofika Ekroni, watu wa Ekroni walipiga kelele, wakasema, Wamelileta hilo sanduku la Mungu wa Israeli kwetu, ili kutuua sisi na watu wetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo, wakalipeleka sanduku hilo la Mungu kwenye mji wa Ekroni. Lakini sanduku hilo la Mungu lilipofika huko, watu wa mji huo walipiga kelele, “Wametuletea sanduku la Mungu wa Israeli ili kutuua sisi na watu wetu.” Biblia Habari Njema - BHND Hivyo, wakalipeleka sanduku hilo la Mungu kwenye mji wa Ekroni. Lakini sanduku hilo la Mungu lilipofika huko, watu wa mji huo walipiga kelele, “Wametuletea sanduku la Mungu wa Israeli ili kutuua sisi na watu wetu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo, wakalipeleka sanduku hilo la Mungu kwenye mji wa Ekroni. Lakini sanduku hilo la Mungu lilipofika huko, watu wa mji huo walipiga kelele, “Wametuletea sanduku la Mungu wa Israeli ili kutuua sisi na watu wetu.” Neno: Bibilia Takatifu Basi wakapeleka Sanduku la Mungu Ekroni. Sanduku la Mungu lilipokuwa linaingia Ekroni, watu wa Ekroni walilia wakisema, “Wamelileta Sanduku la Mungu wa Israeli kwetu ili kutuua sisi na watu wetu.” Neno: Maandiko Matakatifu Basi wakapeleka Sanduku la Mungu Ekroni. Wakati Sanduku la Mungu lilipokuwa linaingia Ekroni, watu wa Ekroni walilia wakisema “Wamelileta Sanduku la Mungu wa Israeli kwetu ili kutuua sisi na watu wetu.” BIBLIA KISWAHILI Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu mpaka Ekroni. Ikawa, sanduku la Mungu lilipofika Ekroni, watu wa Ekroni walipiga kelele, wakasema, Wamelileta hilo sanduku la Mungu wa Israeli kwetu, ili kutuua sisi na watu wetu. |
nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani.
Na Ahazia akaanguka kutoka dirisha la chumba chake ghorofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Nendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.
na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuwapokonya ng'ombe wao.
Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.
Piteni hadi Kalne, mkaone; tena tokea huko nendeni hadi Hamathi iliyo kuu; kisha shukeni hadi Gathi ya Wafilisti; je! Ninyi ni bora kuliko falme hizi? Au eneo lao ni kubwa kuliko eneo lenu?
kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; watawala watano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi,
kisha mpaka ukaendelea hadi upande wa kaskazini wa Ekroni; tena mpaka ulipigwa hadi Shikroni, na kwendelea mpaka kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na ukaishia katika bahari.
Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake.
Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni.
Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya wakuu wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini kote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.
Ikawa, walipolihamisha, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, kwa kuwafadhaisha sana; akawapiga watu wa mjini, wadogo kwa wakubwa, wakapatwa na majipu.