Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Amosi 1:8 - Swahili Revised Union Version

8 Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Nitawang'oa wakazi wa mji wa Ashdodi, pamoja na mtawala wa Ashkeloni. Nitanyosha mkono dhidi ya Ekroni, nao Wafilisti wote waliosalia wataangamia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Nitawang'oa wakazi wa mji wa Ashdodi, pamoja na mtawala wa Ashkeloni. Nitanyosha mkono dhidi ya Ekroni, nao Wafilisti wote waliosalia wataangamia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Nitawang'oa wakazi wa mji wa Ashdodi, pamoja na mtawala wa Ashkeloni. Nitanyosha mkono dhidi ya Ekroni, nao Wafilisti wote waliosalia wataangamia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni. Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,” asema Bwana Mungu Mwenyezi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni. Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,” asema bwana Mwenyezi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.

Tazama sura Nakili




Amosi 1:8
17 Marejeleo ya Msalaba  

Akatoka akapigana na Wafilisti, akauvunja ukuta wa Gathi, na ukuta wa Yabne, na ukuta wa Ashdodi; akajenga miji katika Ashdodi na katikati ya Wafilisti.


Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu;


nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote;


Katika mwaka ule jemadari yule alipofika Ashdodi, alipotumwa na Sargoni mfalme wa Ashuru; naye alipigana na Ashdodi akautwaa;


Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza.


kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani.


Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lolote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.


lakini nitatuma moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake.


Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake.


Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa muali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo.


Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.


Ashkeloni ataona haya na kuogopa; Gaza pia, naye atafadhaika sana; na Ekroni, kwa maana matarajio yake yatatahayarika; na mfalme ataangamia toka Gaza, na Ashkeloni atakuwa hana watu.


Na mwana wa haramu atatawala huko Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.


Hii ndiyo hesabu ya yale majipu waliyoyapeleka wale Wafilisti, yawe matoleo ya kosa kwa BWANA; kwa Ashdodi moja, kwa Gaza moja, kwa Ashkeloni moja, kwa Gathi moja, na kwa Ekroni moja;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo