Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, Ni nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?
1 Samueli 20:32 - Swahili Revised Union Version Yonathani akamjibu Sauli, baba yake, akamwambia, Auawe kwa sababu gani? Amefanya nini? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yonathani akamjibu, “Kwa nini auawe? Amefanya nini?” Biblia Habari Njema - BHND Yonathani akamjibu, “Kwa nini auawe? Amefanya nini?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yonathani akamjibu, “Kwa nini auawe? Amefanya nini?” Neno: Bibilia Takatifu Yonathani akamuuliza baba yake, “Kwa nini auawe? Kwani amefanya nini?” Neno: Maandiko Matakatifu Yonathani akamuuliza baba yake, “Kwa nini auawe? Kwani amefanya nini?” BIBLIA KISWAHILI Yonathani akamjibu Sauli, baba yake, akamwambia, Auawe kwa sababu gani? Amefanya nini? |
Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, Ni nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?
Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.
Akasema, Kwa nini? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulubiwe.
Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua.
Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hadi ukutani. Daudi akaepa, mara mbili.
Naye Yonathani akamsifu Daudi kwa Sauli, babaye akamwambia, Mfalme asikose juu ya mtumishi wake, yaani, juu ya Daudi kwa maana yeye hakukosa juu yako, tena matendo yake kwako yamekuwa mema sana.
Kwa kuwa alihatarisha maisha yake, na kumpiga yule Mfilisti, naye BWANA akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?
Kisha Daudi akatoka Nayothi huko Rama, akakimbia, akaenda kwa Yonathani, akasema mbele yake, Nimefanya nini? Uovu wangu ni nini? Dhambi yangu mbele ya baba yako ni nini, hata akaitaka roho yangu?
Basi, akisema, Ni vema, mimi mtumishi wako nitakuwa na amani; bali akikasirika, ujue ya kuwa amekusudia kutenda jambo baya.
Basi Ahimeleki akamjibu mfalme, akasema, Katika watumishi wako wote ni nani aliye mwaminifu kama Daudi, aliye mkwewe mfalme, tena msiri wako, mwenye heshima nyumbani mwako?