Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 30:2 - Swahili Revised Union Version

2 Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Mtu akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu au akiahidi kwa kiapo na kujifunga nafsi yake kwa ahadi, ni lazima atimize ahadi yake; ni lazima atekeleze yote yale aliyotamka kwa kauli yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Mtu akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu au akiahidi kwa kiapo na kujifunga nafsi yake kwa ahadi, ni lazima atimize ahadi yake; ni lazima atekeleze yote yale aliyotamka kwa kauli yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kisha Mose alizungumza na viongozi wa makabila ya Israeli, akawaambia, “Hili ndilo neno lililoamriwa na Mwenyezi-Mungu:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mwanaume awekapo nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mwanaume awekapo nadhiri kwa bwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.

Tazama sura Nakili




Hesabu 30:2
36 Marejeleo ya Msalaba  

Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.


Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote.


Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote.


Nimeapa nami nikathibitisha, Kuzishika hukumu zako za haki.


Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala kumtenda mwenziwe mabaya, Wala kumsengenya jirani yake.


Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao.


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Mwenzangu amenyosha mkono awadhuru waliopatana naye, Amelivunja agano lake.


Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.


Wekeni nadhiri na mziondoe Kwa BWANA, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa.


Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.


Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu; Na baada ya kuweka nadhiri kuulizauliza habari.


au, kama mtu akijiapisha, kwa kutamka haraka kwa midomo yake, kutenda uovu, au kutenda mema, neno lolote mtu atakalolitamka kwa kiapo pasipo kufikiri, bila kujua; hapo atakapolijua, ndipo atakapokuwa na hatia katika mambo hayo mojawapo;


Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.


Basi Israeli akaweka nadhiri kwa BWANA akasema, Kama wewe utawatia watu hawa mikononi mwangu kweli ndipo mimi nitaiharibu miji yao kabisa.


Tena kama aliweka nadhiri nyumbani mwa mumewe, au kama aliifunga nafsi yake kwa kifungo pamoja na kiapo,


Basi, jengeni miji kwa ajili ya watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; mkayafanye hayo mliotamka kwa vinywa vyenu.


Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga kwa kiapo.


Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga kwa kiapo.


Kulipopambazuka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hadi wamwue Paulo.


Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo.


Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arubaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hadi watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakisubiri kusikia utasemaje.


Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho.


Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kiongozi, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya BWANA huko Mispa.


Basi ikawa mwisho wa hiyo miezi miwili, akarudi kwa babaye, aliyemtenda sawasawa na ile nadhiri yake aliyokuwa ameiweka; naye alikuwa hajamjua mwanamume. Kisha ikawa desturi katika Israeli,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo