Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 30:3 - Swahili Revised Union Version

3 Tena mwanamke atakapomwekea BWANA nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aishi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 “Msichana ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu na kujifunga mwenyewe kwa ahadi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 “Msichana ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu na kujifunga mwenyewe kwa ahadi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 “Mtu akiweka nadhiri kwa Mwenyezi-Mungu au akiahidi kwa kiapo na kujifunga nafsi yake kwa ahadi, ni lazima atimize ahadi yake; ni lazima atekeleze yote yale aliyotamka kwa kauli yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 “Mwanamwali anayeishi bado nyumbani mwa baba yake atakapoweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, ama akajifunga mwenyewe kwa ahadi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 “Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwa bwana, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Tena mwanamke atakapomwekea BWANA nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aishi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake;

Tazama sura Nakili




Hesabu 30:3
10 Marejeleo ya Msalaba  

Tena akamwasi mfalme Nebukadneza, aliyemwapisha kwa Mungu; lakini akajifanyia shingo ngumu, akajitia moyo nguvu asimgeukie BWANA, Mungu wa Israeli.


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtu atakapoondoa nadhiri, hizo nafsi za watu zitakuwa kwa BWANA, kama utakavyowahesabia wewe.


Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.


babaye naye akasikia nadhiri yake, na kile kifungo chake alichofungia nafsi yake, na babaye akamnyamazia; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichofungia nafsi yake kitathibitika.


Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mwanamume au mwanamke atakapoweka nadhiri maalumu, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa BWANA;


Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.


Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu.


Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.


Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo