Tazama, nimemwumba mhunzi afukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.
Zekaria 2:1 - Swahili Revised Union Version Kisha nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Katika maono mengine, nilimwona mtu aliyekuwa na kamba ya kupimia mkononi mwake. Biblia Habari Njema - BHND Katika maono mengine, nilimwona mtu aliyekuwa na kamba ya kupimia mkononi mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Katika maono mengine, nilimwona mtu aliyekuwa na kamba ya kupimia mkononi mwake. Neno: Bibilia Takatifu Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu palikuwa na mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! Neno: Maandiko Matakatifu Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! BIBLIA KISWAHILI Kisha nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake. |
Tazama, nimemwumba mhunzi afukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.
Na kamba ya kupimia itaendelea moja kwa moja hadi katika mlima Garebu, tena itazunguka na kufika Goa.
Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema BWANA. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya BWANA
Akanileta huko, na tazama, alikuwapo mtu, ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba, naye alikuwa na uzi wa kitani mkononi mwake, na mwanzi wa kupimia; akasimama karibu na lango.
Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.
Na alipotoka mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, akielekea mashariki, akapima dhiraa elfu moja, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka katika vifundo vya miguu.
Kisha akapima dhiraa elfu moja, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu moja, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno.
Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa ndani yake, asema BWANA wa majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu.
Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wanaosujudu humo.
Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.