Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 54:16 - Swahili Revised Union Version

16 Tazama, nimemwumba mhunzi afukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 “Tazama, mimi ndiye niliyemuumba mhunzi, afukutaye moto wa makaa na kufua silaha. Ni mimi pia niliyemuumba mwangamizi anayeangamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 “Tazama, mimi ndiye niliyemuumba mhunzi, afukutaye moto wa makaa na kufua silaha. Ni mimi pia niliyemuumba mwangamizi anayeangamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 “Tazama, mimi ndiye niliyemuumba mhunzi, afukutaye moto wa makaa na kufua silaha. Ni mimi pia niliyemuumba mwangamizi anayeangamiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi, yeye afukutaye makaa kuwa moto, na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake. Tena ni mimi niliyemwambia mharibu kufanya uharibifu mwingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Tazama, ni mimi niliyemuumba mhunzi, yeye afukutaye makaa kuwa moto, na kutengeneza silaha inayofaa kwa kazi yake. Tena ni mimi niliyemwambia mharabu kufanya uharibifu mwingi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Tazama, nimemwumba mhunzi afukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.

Tazama sura Nakili




Isaya 54:16
14 Marejeleo ya Msalaba  

lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuoneshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.


BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.


Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.


Je! Hukusikia? Ni mimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale; nikayatimiza sasa, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, ibomoke na kuwa rundo la magofu.


Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.


Tazama, hakika ikiwa utashambuliwa na yeyote, haitakuwa kwa shauri langu. Yeyote atakayekushambulia ataanguka kwa ajili yako.


Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.


Kisha BWANA akanionesha wafua chuma wanne.


Kisha nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake.


naye akamwambia, Nenda mbio ukamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake.


Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana dhambi iliyo kubwa zaidi.


Basi, hakukuwa mhunzi yeyote katika nchi yote ya Israeli; kwa kuwa Wafilisti walisema, Waebrania wasije wakajitengenezea panga au mikuki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo