Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Zekaria 11:2 - Swahili Revised Union Version

Piga yowe, msonobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ombolezeni, enyi misunobari, kwa kuwa mierezi imeteketea. Miti hiyo mitukufu imeharibiwa! Enyi mialoni ya Bashani, ombolezeni, kwa kuwa msitu mnene umekatwa!

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ombolezeni, enyi misunobari, kwa kuwa mierezi imeteketea. Miti hiyo mitukufu imeharibiwa! Enyi mialoni ya Bashani, ombolezeni, kwa kuwa msitu mnene umekatwa!

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ombolezeni, enyi misunobari, kwa kuwa mierezi imeteketea. Miti hiyo mitukufu imeharibiwa! Enyi mialoni ya Bashani, ombolezeni, kwa kuwa msitu mnene umekatwa!

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Piga yowe, ee msunobari, kwa kuwa mwerezi umeanguka; miti ya fahari imeharibiwa! Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, msitu mnene umefyekwa!

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Piga yowe, ee mti wa msunobari, kwa kuwa mwerezi umeanguka; miti ya fahari imeharibiwa! Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, msitu mnene umefyekwa!

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Piga yowe, msonobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Zekaria 11:2
12 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanadamu, uelekeze uso wako kusini, ukadondoze neno lako upande wa kusini, ukatabiri juu ya msitu wa uwanda wa Negebu,

kwa mialoni ya Bashani wamefanya makasia yako; na sitaha zako wamezifanya kwa pembe iliyotiwa kazi ya njumu katika mti wa mihugu itokayo Kitimu.

Hao nao waliteremka kuzimuni pamoja naye kwa watu waliouawa kwa upanga; naam, wale waliowasaidia, waliokaa chini ya uvuli wake kati ya mataifa.

Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na hao wanaokaa salama katika mlima wa Samaria, watu mashuhuri wa taifa lililo la kwanza, ambao nyumba ya Israeli huwaendea.

Ifungue milango yako, Ee Lebanoni, Ili moto uiteketeze mierezi yako.

Sikiza, maombolezo ya wachungaji, Kwa maana utukufu wao umeharibiwa; Sikiza, ngurumo za simba, Kwa maana vichaka vya Yordani vimeharibiwa!

Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?