Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
Zekaria 1:5 - Swahili Revised Union Version Je, Baba zenu wako wapi? Je, manabii nao wanaishi milele? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazee wenu, wako wapi? Na manabii, je, wanaishi milele? Biblia Habari Njema - BHND Wazee wenu, wako wapi? Na manabii, je, wanaishi milele? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazee wenu, wako wapi? Na manabii, je, wanaishi milele? Neno: Bibilia Takatifu Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? Neno: Maandiko Matakatifu Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? BIBLIA KISWAHILI Je, Baba zenu wako wapi? Je, manabii nao wanaishi milele? |
Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.
Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani.
Haya! Twaa wewe gombo lingine, ukaandike ndani yake maneno yote ya kwanza, yaliyokuwa katika gombo la kwanza, ambalo Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ameliteketeza.
Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Abrahamu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.
Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.