Zaburi 3:2 - Swahili Revised Union Version Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wengi wanasema juu yangu, “Hatapata msaada kwa Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Wengi wanasema juu yangu, “Hatapata msaada kwa Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wengi wanasema juu yangu, “Hatapata msaada kwa Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” Neno: Maandiko Matakatifu Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” BIBLIA KISWAHILI Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. |
Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?
Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito.