Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 139:1 - Swahili Revised Union Version

Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenichunguza; wewe wanijua mpaka ndani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ee Mwenyezi Mungu, umenichunguza na kunijua.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ee bwana, umenichunguza na kunijua.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 139:1
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na mimi, Daudi, nikuambie nini tena zaidi? Iwapo wewe umemjua mtumishi wako, Ee Bwana MUNGU.


basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote);


Lakini nakujua, kuketi kwako, na kutoka kwako, na kuingia kwako; na ghadhabu yako unayonighadhibikia.


Na Daudi akuambie nini tena zaidi kwa habari ya heshima aliyotendewa mtumishi wako? Kwa maana wewe umemjua mtumishi wako.


Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.


Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;


Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,


Je! Mungu hangegundua jambo hilo? Maana ndiye azijuaye siri za moyo.


Lakini wewe, BWANA, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.


Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.


Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.


Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama muali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.


nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.