Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 12:3 - Swahili Revised Union Version

3 Lakini wewe, BWANA, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua; wayathibiti maelekeo yangu kwako. Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa, watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua; wayathibiti maelekeo yangu kwako. Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa, watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua; wayathibiti maelekeo yangu kwako. Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa, watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Hata hivyo unanijua mimi, Ee Mwenyezi Mungu; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaoenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Hata hivyo unanijua mimi, Ee bwana; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Lakini wewe, BWANA, wanijua; umeniona, umeujaribu moyo wangu, jinsi unavyokuelekea; uwakokote kama kondoo waendao kuchinjwa, ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.

Tazama sura Nakili




Yeremia 12:3
23 Marejeleo ya Msalaba  

Nakusihi, BWANA, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.


Nami ninajua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao.


Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.


BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu.


Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;


Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,


Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.


Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na fikira Ndiye Mungu aliye mwenye haki.


Ee BWANA, unajua wewe; unikumbuke, unijie, ukanilipizie kisasi juu yao wanaoniudhi; usiniondoe kwa uvumilivu wako; ujue ya kuwa ni kwa ajili yako nilivyopatikana na matukano.


Mimi hapa sikufanya haraka kuacha kuwa mchungaji nyuma yako; wala sikuitamani siku ya maradhi ya kuua; wewe unajua; yaliyotoka midomoni mwangu yalikuwa mbele za uso wako.


Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.


Lakini, Ee BWANA wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona fikira na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.


Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wameteremka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.


Wachinjeni mafahali wake wote; Na wateremkie machinjoni; Ole wao! Maana siku yao imewadia, Wakati wa kujiliwa kwao.


Nao wataanguka, wakiwa wameuawa, katika nchi ya Wakaldayo, wakiwa wametumbuliwa katika njia zake kuu.


Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.


Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejinenepesha mioyo yenu kama kwa siku ya kuchinjwa.


Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo