Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu, Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.
Zaburi 102:6 - Swahili Revised Union Version Nimekuwa kama ndege wa jangwani, Na kufanana na bundi katika mahame. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimekuwa kama ndege wa jangwani; kama bundi kwenye mahame. Biblia Habari Njema - BHND Nimekuwa kama ndege wa jangwani; kama bundi kwenye mahame. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimekuwa kama ndege wa jangwani; kama bundi kwenye mahame. Neno: Bibilia Takatifu Nimekuwa kama bundi wa jangwani, kama bundi kwenye magofu. Neno: Maandiko Matakatifu Nimekuwa kama bundi wa jangwani, kama bundi kwenye magofu. BIBLIA KISWAHILI Nimekuwa kama ndege wa jangwani, Na kufanana na bundi katika mahame. |
Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu, Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.
Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi; Nitaomboleza kama mbweha, Na kulia kama mbuni.
Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; bundi na kunguru watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.
Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;