Zaburi 102:3 - Swahili Revised Union Version Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku zangu zapita kama moshi; mifupa yangu yaungua kama katika tanuri. Biblia Habari Njema - BHND Siku zangu zapita kama moshi; mifupa yangu yaungua kama katika tanuri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku zangu zapita kama moshi; mifupa yangu yaungua kama katika tanuri. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi; mifupa yangu inaungua kama kaa la moto. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi, mifupa yangu inaungua kama kaa la moto. BIBLIA KISWAHILI Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga. |
Usinifiche uso wako, Usimkatalie mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.
Maana maisha yangu yamekwisha kwa huzuni, Na miaka yangu kwa maumivu. Nguvu zangu zimeniishia kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imepooza.
Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.
Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu, Nao umeishinda; Ametandika wavu aninase miguu, Amenirudisha nyuma; Amenifanya kuwa mtu wa pekee, Na mgonjwa mchana kutwa.
lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.