Lakini ukitaka kwenda, haya, jitie nguvu upigane; Mungu atakuangusha mbele ya adui; maana Mungu anazo nguvu za kusaidia, na kuangusha.
Zaburi 102:10 - Swahili Revised Union Version Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako; Maana umeniinua na kunitupilia mbali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kwa sababu ya ghadhabu na hasira yako, maana umeniokota na kunitupilia mbali. Biblia Habari Njema - BHND kwa sababu ya ghadhabu na hasira yako, maana umeniokota na kunitupilia mbali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kwa sababu ya ghadhabu na hasira yako, maana umeniokota na kunitupilia mbali. Neno: Bibilia Takatifu kwa sababu ya ghadhabu yako kuu, kwa maana umeniinua na kunitupa kando. Neno: Maandiko Matakatifu kwa sababu ya ghadhabu yako kuu, kwa maana umeniinua na kunitupa kando. BIBLIA KISWAHILI Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako; Maana umeniinua na kunitupilia mbali. |
Lakini ukitaka kwenda, haya, jitie nguvu upigane; Mungu atakuangusha mbele ya adui; maana Mungu anazo nguvu za kusaidia, na kuangusha.
Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.
Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili.
Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.
Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;