akamweka awe mfalme wa Gileadi, na Waasheri, na Yezreeli, na Efraimu, na Benyamini, na juu ya Israeli wote.
Yoshua 16:5 - Swahili Revised Union Version Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu, Biblia Habari Njema - BHND Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa kabila la Efraimu kulingana na jamaa zao walipata sehemu yao ambayo mpaka wake upande wa mashariki ulipita Ataroth-adari hadi Beth-horoni ya Juu, Neno: Bibilia Takatifu Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, kufuatana na koo zao: Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu, Neno: Maandiko Matakatifu Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu, BIBLIA KISWAHILI Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kufuata jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu; |
akamweka awe mfalme wa Gileadi, na Waasheri, na Yezreeli, na Efraimu, na Benyamini, na juu ya Israeli wote.
Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.
Na hizi ndizo miliki yao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;
Na mpakani mwa Manase, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Efraimu, fungu moja.
BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hadi kufikia Azeka, tena hadi kufikia Makeda.
kisha ikatoka huko Betheli kwendelea Luzu, kisha ikaendelea hata kuufikia mpaka wa Waarki mpaka Atarothi;
Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukateremkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini.