Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani mwa mashariki.
Yoshua 13:8 - Swahili Revised Union Version Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyowapa; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makabila ya Reubeni, Gadi na nusu nyingine ya kabila la Manase yalikuwa yamepewa nchi iliyo mashariki ya mto Yordani, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose, mtumishi wake. Biblia Habari Njema - BHND Makabila ya Reubeni, Gadi na nusu nyingine ya kabila la Manase yalikuwa yamepewa nchi iliyo mashariki ya mto Yordani, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose, mtumishi wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makabila ya Reubeni, Gadi na nusu nyingine ya kabila la Manase yalikuwa yamepewa nchi iliyo mashariki ya mto Yordani, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose, mtumishi wake. Neno: Bibilia Takatifu Ile nusu nyingine ya Manase, Wareubeni na Wagadi, walishapokea urithi Musa aliokuwa amewapa mashariki mwa Yordani, sawasawa na mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyowagawia. Neno: Maandiko Matakatifu Ile nusu nyingine ya Manase, Wareubeni na Wagadi, walishapokea urithi Musa aliokuwa amewapa mashariki mwa Yordani, sawasawa na mtumishi wa bwana alivyowagawia. BIBLIA KISWAHILI Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyowapa; |
Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani mwa mashariki.
Tukaitwaa na nchi wakati huo, katika mikono ya hao wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ng'ambo ya Yordani, kutoka bonde la Arnoni mpaka kilima cha Hermoni;
Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki;
Musa mtumishi wa BWANA na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa BWANA akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila la Manase iwe urithi wao.
Basi sasa gawanya nchi hii, iwe urithi wa hizi kabila tisa, na nusu ya kabila la Manase.
kutoka huko Aroeri, iliyoko pale ukingoni mwa bonde la Amoni, na huo mji ulioko pale katikati ya bonde, na nchi tambarare yote ya Medeba mpaka Diboni;
Na sasa yeye BWANA, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani.
Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila la Manase, wakavuka, wakiwa wamebeba silaha mbele ya wana wa Israeli, kama Musa alivyowaambia;
Hata baadhi ya Waebrania walivuka Yordani, wakaingia nchi ya Gadi na Gileadi; lakini Sauli alikuwa angali huko Gilgali, nao watu wote wakamfuata wakitetemeka.