Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 32:19 - Swahili Revised Union Version

19 Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani mwa mashariki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Hatutamiliki mali yoyote miongoni mwao ngambo ya mto Yordani, kwa sababu sisi tumepata maeneo yetu ngambo hii, mashariki ya mto Yordani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Hatutamiliki mali yoyote miongoni mwao ngambo ya mto Yordani, kwa sababu sisi tumepata maeneo yetu ngambo hii, mashariki ya mto Yordani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Hatutamiliki mali yoyote miongoni mwao ng'ambo ya mto Yordani, kwa sababu sisi tumepata maeneo yetu ng'ambo hii, mashariki ya mto Yordani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ng’ambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki mwa Yordani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ng’ambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa mashariki mwa Yordani.

Tazama sura Nakili




Hesabu 32:19
11 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao.


Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.


Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.


hayo makabila mawili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea maawio ya jua.


Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyowapa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo