Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.
Yona 2:7 - Swahili Revised Union Version Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nilimkumbuka BWANA; Maombi yangu yakakufikia, Katika hekalu lako takatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Roho yangu ilipoanza kunitoka, nilikukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, sala yangu ikakufikia, katika hekalu lako takatifu. Biblia Habari Njema - BHND Roho yangu ilipoanza kunitoka, nilikukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, sala yangu ikakufikia, katika hekalu lako takatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Roho yangu ilipoanza kunitoka, nilikukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu, sala yangu ikakufikia, katika hekalu lako takatifu. Neno: Bibilia Takatifu “Uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, Mwenyezi Mungu, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu. Neno: Maandiko Matakatifu “Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, bwana, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu. BIBLIA KISWAHILI Roho yangu ilipozimia ndani yangu, Nilimkumbuka BWANA; Maombi yangu yakakufikia, Katika hekalu lako takatifu. |
Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu.
Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako.
Katika shida yangu nilimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumainie Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Maana nitamsifu tena, Aliye msaada wangu, Na Mungu wangu.
Heri mtu yule umchaguaye, Na kumkaribisha akae nyuani mwako. Na tushibe wema wa nyumba yako, Patakatifu pa hekalu lako.
Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.
Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako; Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.
Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.
Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili upinzani mkuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.