Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.
Yohana 8:4 - Swahili Revised Union Version Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha wakamwuliza Yesu, “Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwa katika uzinzi. Biblia Habari Njema - BHND Kisha wakamwuliza Yesu, “Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwa katika uzinzi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha wakamwuliza Yesu, “Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwa katika uzinzi. Neno: Bibilia Takatifu Wakamwambia Isa, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Neno: Maandiko Matakatifu Wakamwambia Isa, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. BIBLIA KISWAHILI Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. |
Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.
Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.
Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake kama hawa; nawe wasemaje?
Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli.
Kisha mumewe akaondoka akamfuata, aseme naye kwa upendo, ili apate kumrudisha tena, naye alikuwa na mtumishi wake pamoja naye na punda kadhaa; huyo mwanamke akamkaribisha katika nyumba ya baba yake; naye baba yake alipomwona akafurahi kuonana naye.