Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 1:19 - Swahili Revised Union Version

19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Yosefu, mumewe, kwa vile alikuwa mwadilifu, hakutaka kumwaibisha hadharani; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, hivyo basi alikusudia kumwacha kwa siri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa, alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, bali aliazimu kumwacha kwa siri.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

Tazama sura Nakili




Mathayo 1:19
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mke wa mwana wako, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.


Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.


Tena mtu yeyote alalaye na mwanamke aliye mjakazi, naye ameposwa na mwanamume mwingine, wala hakukombolewa kwa lolote, wala hakupewa uhuru wake; watachunguzwa; hawatauawa, kwa sababu huyo mwanamke hakuwa huru.


Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.


Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.


Maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha.


Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.


Wakasema, Kornelio jemadari, mtu mwenye haki, mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, ili asikilize kile utakachosema.


Kulipokucha hawakuitambua ile nchi, ila waliona hori yenye ufuo, wakashauriana kuiegesha merikebu huko, kama ikiwezekana.


Nami nikiwa na tumaini hilo nilitaka kufika kwenu hapo kwanza, ili mpate karama ya pili;


Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo