Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.
Yohana 8:27 - Swahili Revised Union Version Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hawakuelewa kwamba Yesu alikuwa akisema nao juu ya Baba. Biblia Habari Njema - BHND Hawakuelewa kwamba Yesu alikuwa akisema nao juu ya Baba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hawakuelewa kwamba Yesu alikuwa akisema nao juu ya Baba. Neno: Bibilia Takatifu Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia kuhusu Baba yake wa Mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia juu ya Baba yake wa Mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba. |
Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.
Naye akaniambia, Nenda, ukawaambie watu hawa, Endeleeni kusikia, lakini msifahamu; endeleeni kutazama, lakini msione.
Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenituma ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.
Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.
Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.