Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yohana 8:26 - Swahili Revised Union Version

26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenituma ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Nina mambo mengi ya kusema kuwahusu ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kuaminika, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Nina mambo mengi ya kusema juu yenu na mengi ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kweli, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenituma ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.

Tazama sura Nakili

Yohana 8:26
17 Marejeleo ya Msalaba  

Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.

Hata bado ningali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamuwezi kuyastahimili hivi sasa.

Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nilitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.

Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo tunalinena, na lile tuliloliona tunalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali.

Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenituma.

Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenituma ni wa kweli, msiyemjua ninyi.

Basi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Hasa neno lilo hilo ninalowaambia.

Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba.

Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Abrahamu hakufanya hivyo.

Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si Ndiyo na Siyo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo