Basi, lisikieni neno la BWANA, enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu.
Yohana 7:49 - Swahili Revised Union Version Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini umati huu haujui sheria ya Mose; umelaaniwa!” Biblia Habari Njema - BHND Lakini umati huu haujui sheria ya Mose; umelaaniwa!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini umati huu haujui sheria ya Mose; umelaaniwa!” Neno: Bibilia Takatifu Lakini umati huu wa watu wasiojua Torati ya Musa, wamelaaniwa.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini huu umati wa watu wasiojua Torati ya Musa, wamelaaniwa.” BIBLIA KISWAHILI Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa. |
Basi, lisikieni neno la BWANA, enyi watu wenye dharau, mnaowatawala watu hawa walio ndani ya Yerusalemu.
Ole wao walio na hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!
watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa.
Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.
Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?