Yohana 7:44 - Swahili Revised Union Version Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakuna aliyejaribu kumkamata. Biblia Habari Njema - BHND Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakuna aliyejaribu kumkamata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakuna aliyejaribu kumkamata. Neno: Bibilia Takatifu Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa. Neno: Maandiko Matakatifu Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa. BIBLIA KISWAHILI Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika. |
Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.
Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.