Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Yohana 6:59 - Swahili Revised Union Version Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sunagogi kule Kafarnaumu. Biblia Habari Njema - BHND Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sunagogi kule Kafarnaumu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sunagogi kule Kafarnaumu. Neno: Bibilia Takatifu Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu. Neno: Maandiko Matakatifu Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu. BIBLIA KISWAHILI Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu. |
Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.
wakapanda katika mashua, wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaumu. Nako kumekwisha kuwa giza, wala Yesu hajawafikia.
Basi mkutano, walipoona ya kuwa Yesu hayuko huko wala wanafunzi wake, waliingia mashuani wenyewe, wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu.